Categories
Neno la Mungu

Vipimo vya Mungu juu ya kazi zetu siku ya hukumu

_____________________________________

Mtume Paulo anaeleza kuwa kazi zetu (kama waamini au watumishi wa Mungu) zitapimwa na “moto”, yaani zitawekwa chini ya kipimo cha Mungu ili kuonyesha kama ni thabiti, safi, na za kweli. Hii haizungumzii wokovu kwa matendo, bali tuzo au thawabu kwa uaminifu wetu katika huduma na maisha ya kila siku.

1 Wakorintho 3:13 (SUV):
“Kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri; maana siku ile itaiweka wazi, kwa sababu yafunuliwa katika moto; na ule moto utaijaribu kazi ya kila mtu, ya namna gani ilivyo.”

Ubora, si wingi – Mungu haangalii tu kiasi cha kazi, bali ubora wa moyo na uaminifu wetu 
(Kol. 3:23).

Fikiri kwa kina mambo haya:

1. Motisha ya ndani – Je, tulifanya kwa ajili ya sifa, fedha, au kwa upendo wa Mungu? (Mathayo 6:1-4).

2. Uaminifu katika kazi ndogo na kubwa (Luka 16:10).

3. Uaminifu katika nafasi yako – Ulimtumikia Mungu wapi? Na alikuita kwa kusudi hilo? Na je ulikua mwaminifu kwa kazi hiyo aliyokuitia? (1 Petro 4:10).

Pastor Aloyce

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *