Categories
Neno la Mungu

Uaminifu wa mwanaume kwa mke na familia yake

Katika zama ambazo uaminifu unaonekana kama kitu cha kizamani, mwanaume mwaminifu amebaki kuwa kielelezo cha heshima, uaminifu kwa Mungu, na msingi wa familia yenye nguvu. Uaminifu hauhusu tu kutozini, bali ni hali ya moyo unaojitoa kikamilifu kwa mke wake – kimwili, kihisia, na kiroho. Hii ni silaha dhidi ya kuvunjika kwa ndoa na kizazi.

1. Neno la Mungu linasemaje juu ya uaminifu

Waefeso 5:25
“Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa na kujitoa kwa ajili yake.”

Uaminifu ni wito wa kiroho. Ni agizo la Mungu ambalo mwanaume analo si kwa sababu ya hali ya ndoa, bali kwa sababu ya kumtii Mungu.

Mithali 5:15-18
“Kunywa maji ya birika lako mwenyewe… chemchemi yako ibarikiwe, nawe umfurahie mke wa ujana wako.”

“Wanaume wa kweli hujua kuwa uaminifu ni chaguo la kila siku – si hali ya hisia.” — Dr. Tony Evans

Ona shuhuda hizi

“Nilipoanza ndoa, sikuwa na uelewa wa maana ya uaminifu wa kihisia. Nilidhani kama sijazini basi mimi ni mwaminifu. Lakini baada ya mke wangu kunikamata nikichati kimapenzi na mwanamke wa kazini, ndoa yetu ilianza kuyumba. Iliniuma sana. Nililazimika kujifunza tena kupenda na kuonyesha uwazi. Leo hii ndoa yetu imepona.”

“Nimeishi na mke wangu kwa miaka 41. Sio kwamba hakuna vishawishi. Lakini nilijifunza kuwa moyo wa mke wangu ni dhamana ya Mungu kwangu. Nilivyoamua kuilinda ndoa yangu, ndivyo baraka zilivyoongezeka.”

Kitabu hiki kiko jikoni, soon nitakitoa kwa Neema ya Mungu!

Pastor Aloyce J Aloyce

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *